Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. George Mkuchika, ametangaza kuwashughulikia wakuu wa mikoa na wilaya ambao wanavunja sheria za utumishi kwa kuwafukuzisha kazi watumishi ambao hawawaajiri wao.
Leo katika kikao cha 52 cha bunge la 11, Kapt. Mkuchika ameyasema hayo ambapo ameeleza kuwa kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma, muajiri ndiye mwenye mamlaka ya kutoa adhabu au kufukuza lakini siyo mtu mwingine yoyote.
Maelezo hayo yamekuja wakati Kapt. Mkuchika akijibu swali la Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini wakati akiuliza kuhusu "Awamu hii kumezuka tabia ya baadhi ya wakuu wa wilaya na mikoa kuwavua vyeo baadhi ya waalimu pamoja na kuwafukuza kazi kinyume kutokana na sababu kama shule kutofanya vizuri nk. Hali inavyoendelea inaonekana ni kama hatua mahsusi zilizoagizwa na serikalini zimependekezwa"
Mh. Selasini amehoji "Je, serikali ipo tayari kufanya mapitio ya maamuzi yote hayo na kuwarejeshea vyeo vyao pamoja na ajira madaktari na waalimu iwapo wataonekana kuwa wameonewa?
Akijibu swali hilo. Kapt Mkuchika amesema "Nchi hii inaendeshwa kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni. Kwa taratibu za kiutumishi aliyekuajiri ndiye mwenye mamlaka ya kuadhibu na ndiye anayekufukuza. Wanaotajwa hapo mara nyingi wanapogundua kuwa wamefanya makosa, wanamsimamisha wakati wanamsubiri yule mwenye mamamlaka ya ajira achukue hatua za mwisho".
Ameomngeza "Mh. Spika kupitia bunge lako, naomba niseme Aliyekuajiri wewe ndiye mwenye madaraka ya kukufukuza. Kama kuna mahala mtumishi yoyote amefukuzwa kazi na Mkuu wa mkoa au wilaya naomba niletewe suala hilo nitalishughulikia mara moja".
Pamoja na hayo Kapt. Mkuchika ameseme kuwa Viongozi huwa wanapatiwa mafunzo "Kama mnafuatilia sasa hivi mambo yametulia, maji yametulia kwenye mtungi siyo kama tulivyoanza huko".
Chanzo- EATV