Ikiwa zimebaki siku nne kabla ya kuanza kwa mashindano ya kombe la Dunia nchini Urusi, kampuni ya michezo Gracenote imetoa michezo mitano ya kombe la Dunia ambayo ilitoa matokeo ambayo hayakutarajiwa na wapenzi wa soka.
Michezo ifuatayo ndiyo ilitoa matokeo ya kushangaza zaidi tangu kuanzishwa kwa mashindano ya kombe la Dunia kwa mujibu wa Gracenote.
5. Uruguay 2-1 Brazil 1950
Mchezo huu unashika nafasi ya tano ni kati Uruguay dhidi ya Brazil katika mashindano yaliyofanyika mwaka 1950 nchini Brazil. timu ya Uruguay ilishangaza wapenzi wa soka duniani baada ya kufanikiwa kuwafunga wenyeji 2-1
Uruguay ilikuwa na asilimi 14.3 za uwezekano wa kushinda mechi hiyo huku Brazil ikihitaji alama moja kuweza kuwa mabingwa ilijikuta ikikabidhi ubingwa kwa Uruguay.
4. Ghana 2-0 Jamhuri ya Czech 2006
Ikiwa imepewa asilimia 13.9 za kushinda mechi Ghana, ilishangaza dunia kwa kuifunga Jamhuri ya Czech 2-0 katika kombe la dunia lililofanyika nchini Ujerumani mwaka 2006, matokeo hayo yaliwezesha timu ya Ghana kusonga mbele katika hatua ya 16 bora baada ya kushika nafasi ya pili katika kundi E nyuma ya Italy.
3. Algeria 2-1 Ujerumani Magharibi 1982
Kwa mujibu wa utafiti huo unaonesha kuwa mchezo huwa umeshika nafasi ya tatu katika matokeo ya kushangaza zaidi katika mashindano yaliyofanyika nchini Hispania. wakiwa katika kundi la pili, Algeria walikuwa na asilimia 13.1 tu ya kushinda lakini iliwafunga Ujerumani Magharibi 2-1.
2. Uswizi 1-0 Hispania 2010
Mashindano yaliyofanyika nchini Afrika Kusini, licha ya ubora wa kikosi cha Hispania lakini walijikuta wakipoteza mchezo dhidi ya Uswizi kwa kubali kipigo goli 1-0 katika mechi ya kwanza kundi G. Uswizi walikuwa na asilimia 10.3 za kushinda mechi hiyo.
1. Marekani 1-0 England 1950
Mchezo ulioshika nafasi ya kwanza ni mashindano ya kombe la Dunia yaliyofanyika nchini Brazil, Marekani iliifunga England goli 1-0 katika uwanja Belo Horizonte na Marekani ilikuwa na asilimia 9.5 za uwezekano wa kuifunga England kwa wakati huo.
Social Plugin