Watu 20 wamefariki na wengine 45, kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha Hiace 3 na Lori lililokuwa limebeba Kontena maeneo ya Mbalizi mkoani Mbeya ambapo kati ya watu hao wanawake ni 12 na wanaume 8.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Mussa Taibu amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana, na uchunguzi unaendelea.
“Ajali hii imehusisha Lori na daladala tatu katika Mlima Iwambi mkaoni hapa na kuzipelekea kudumbukia mtoni , ambapo vifo mpaka sasa ni watu ishirini na majeruhi ni arobaini na tano wamepelekwa katika hospitali ya rufaa ya Mbeya”, amesema Kamanda.
Kamanda ameongeza kuwa jiografia ya eneo hilo imechangia ajali mara kwa mara katika eneo hilo, na kuwasihi madereva kuwa makini na kupunguza mwendo barabarani.
TAZAMA PICHA NYINGI ZAIDI HAPA
TAZAMA PICHA NYINGI ZAIDI HAPA
Social Plugin