Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga linamshikilia Emmanuel Chilunda (36) mkazi wa Dar es salaam baada ya kukamatwa akisafirisha magunia mawili ya bangi yenye kilo 80 kutoka kijiji cha Nhumba halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule amesema mtuhumiwa alikamatwa Julai 8,2018 majira ya moja na nusu usiku katika eneo la daraja la Manonga kijiji cha Isaka,kata ya Isaka,wilaya ya Kipolisi Msalala barabara ya Kahama - Tinde.
"Tulimkamata Emmanuel Chilunda ambaye ni dereva akiwa na kilo 80 za bangi kwenye gari aina ya DAF lenye namba za usajili T.590 BZA lenye tela namba T.668 CBD",
"Mbinu iliyotumiwa na dereva ni kupakia bangi kwa kuchanganya na mizigo mingine ya pamba,tunaendelea kumhoji huyu mtuhumiwa na tutamfikisha mahakamani baada ya uchunguzi wa awali kukamilika",amesema kamanda Haule.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule akipanda juu ya lori lililokuwa limepakia magunia ya bangi na pamba
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule na maafisa wengine wa polisi wakiangalia gunia la bangi
Social Plugin