AZAM FC YAWEKA WAZI LINI SHAABAN IDD ATATUA HISPANIA


Mchezaji Shaaban Idd mwenye jezi nyeupe kwenye moja ya mechi za timu yake.

Klabu ya soka ya Azam FC kupitia kwa meneja wake Phillip Alando, imesema mshambuliaji wao Shaaban Idd ambaye amesajiliwa na timu ya Tenerife ya Hispania, ataondoka nchini mara baada ya michuano ya Kombe la Kagame.

Akiongea leo na eat.tv meneja huyo amesema kila kitu kimeshawekwa sawa kati ya Azam FC na Tenerife FC, hivyo mchezaji huyo ataondoka hivi karibuni baada ya michuano ya Kombe la Kagame ambayo inaendelea hapa nchini huku Azam FC akiwa ndio bingwa mtetezi.

''Shaaban tayari ana mkataba wake na Tenerife na taratibu zote ameshakamilisha, kilichobaki ni kumaliza kuitumikia klabu yetu kwenye michuano ya Kagame kisha asafiri kwenda Hispania kwaajili ya kuanza maisha mapya ya soka la kimataifa'', amesema Alando.

Shaaban Idd anaungana na nyota mwingine wa Tanzania anayechezea timu hiyo, Farid Mussa. Alando ameongeza kuwa wao kama timu wataendelea kuendeleza vipaji hata kama timu hazitawanunua moja kwa moja lakini kwa vipaji vya nyota hao wataendelea kuwaruhusu wakacheze kwa mkop

Mshambuliaji huyo amesaini mkataba miaka 2 kucheza kwa mkopo ndani ya Tenerife. Msimu uliopita klabu ya Tenerife ilimaliza katika nafasi ya 11 kwenye ligi daraja la pili ya Hispania maarufu kama 'Segunda B' ambayo washindi watatu huwa wanapanda ligi kuu.
Chanzo- EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post