Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Breaking : MBUNGE STEPHEN NGONYANI 'PROFESA MAJI MAREFU' AFARIKI DUNIA


Mbunge wa Korogwe Vijijini mkoani Tanga Stephen Ngonyani ' Profesa Majimarefu' (CCM) amefariki dunia leo usiku Jumatatu Julai 2,2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Taarifa ya kifo cha mbunge huyo imethibitishwa na ofisa uhusiano wa Muhimbili, Aminiel Eligaeshi.

Juni 20, 2018 Majimarefu alihamishiwa kwa ndege kutoka mkoani Dodoma kwenda MNH kwa matibabu. 

Hata hivyo kilichokuwa kikimsumbua mbunge huyo hakikuwekwa wazi.

Juni 6, 2018 mbunge huyo alifiwa na mkewe, Mariam aliyekuwa akipatiwa matibabu MNH. 

Bunge la Tanzania limeendelea kupoteza wabunge ambapo kifo cha Profesa Majimarefu kinafanya idadi ya wabunge hao kufikia watano.

Wabunge wengine waliofariki dunia ni Dkt. Elly Macha (Viti Maalumu) na Kasuku Bilago (Buyungu) wote wa Chadema. wengine ni Leonidas Gama (Songea Mjini) na Hafidh Ali Tahir (Dimani) wa CCM.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com