Rais Abdel- Fattah el- Sissi
Bunge la Misri limepitisha sheria tata inayolenga kudhibiti mitandao maarufu ya kijamii inayochapisha habari za uongo.
Mswada huo uliopitishwa Jumatatu wiki hii unaliwezesha bunge kuzuia akaunti binafsi ya mtu katika mitandao ya kijamii iliyo na wafuasi zaidi ya 5,000 kutokana na kuchapisha taarifa za uongo.
Hata hivyo muswada huo lazima usainiwe na Rais Abdel- Fattah el- Sissi ili uwe sheria.
Chini ya utawala wa el-Sissi Misri imewatia mabaroni , kuwashitaki na kuwafunga waandishi wa habari kutokana na makosa ya mitandao ya kijamii.
Iwapo muswada huo uatasainiwa kuwa sheria baraza la juu la habari nchini humo litasimamia akaunti maarufu katika mitandao ya kijamiii zitakazokuwa zikiendeshwe kama vyombo vya habari.
Waandishi wa habari wasio na mipaka waliitaja Misri kuwa ya 161 kati ya nchi 181 kwenye orodha yake ya mwaka 2017 ya Uhuru wa vyombo vya habari.