Chama Cha Mapinduzi kimetangaza kuvuna wanachama 170 wa upinzani wilaya ya Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro, huku kikijigamba kwamba tukio hilo ni ishara ya kuvunja ngome ya Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR- Mageuzi).
Mbatia aliibuka mshindi katika uchaguzi wa mwaka 2015 na kuwabwaga, washindani wake wa karibu, Innocent Melleck Shirima (CCM) na Augustino Mrema (TLP).
Wanasiasa hao wamedaiwa kupokelewa na Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Jonathan Mabihya katika kata ya Njiapanda Mashariki.
Wanachama wanaodaiwa kutoka vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi pamoja na CUF katika mkoa huo.Akizungumza baada ya kuwapokea wanachama hao na kuwapa kadi za CCM, Mabihya aliwapongeza kwa maamuzi waliyochukua.
Kwa upande wake, Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Moshi vijijini, Hussein Jamal alisema wilaya hiyo ina majimbo mawili ya Vunjo na Moshi vijijini.