Watoto waliokwama pangoni wakiwa katika picha ya pamoja.
Wapiga mbizi nchini Thailand kwa kushirikiana na wengine kutoka nje ya nchi wamefanikiwa kuwaokoa watoto wanne na kufanya idadi ya waliookolewa kutoka katika pango kufikia nane.
Vijana hao 12 na kocha wao wa soka walikwama ndani ya pango tangu Juni 23, 2018 baada ya mvua kubwa kusababisha mafuriko ambapo maji yalijaa sehemu mbalimbali katika pango na kusababisha watoto hao kushindwa kutoka nje.
Wanajeshi wa majini wa Thailandi wanaoongoza operesheni hiyo wamethibitisha taarifa hizo na kudai kuwa watoto hao wamepelekwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi
Kikosi cha uokoaji nchini Thailand kimeendelea kutumia mashine za kuvuta maji kutoka ndani ya pango ilo ili kurahisisha operesheni hiyo huku takwimu za utabiri wa hali ya hewa ukionesha kuwa mvua zitaongezeka kunyesha nchini humo.
Aidha, Mkuu wa Kikosi cha Uokoaji ambaye ni Gavana wa Jimbo ‘Chang Raju,’ Narongsak Osottanakorn amesema kuwa uokoaji huo wenye mazingira ya hatari utawachukua takribani siku nne kutegemeana na hali ya hewa.
Social Plugin