Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaalika viongozi wakuu wastaafu wote nchini kwa ajili ya kufanya nao mazungumzo leo Jumanne Julai 03, 2018 Ikulu jijini Dar es saalam.
Viongozi hao ni Marais, Makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu, Maspika na Majaji Wakuu. Hii ni mara ya kwanza kwa viongozi hao kukutana na rais ikulu.
Alichokisema Rais Magufuli:
Wazee wangu karibuni sana. Nmeamua kuwakaribisha sababu nyie ni wazee wetu ambao mumeitumikia nchi katika vipindi mbalimbali na hapa Ikulu ni kwenu.
Nimewaita tukae tuzungumze tushauriane ili tujue tunaelekea wapi, Nahitaji ushauri wa wazee.
Na ninyi pia inaweza kuwa ni nafasi nzuri kwa wazee waliolitumikia taifa kwa nafasi mbalimbalimbalimbali kusema neno.
Nimewaita ninyi wazee wangu, bahati nzuri ninyi wote nimefanya kazi na nyie katika kipindi chenu tofauti. Mkapa ulinichagua naibu Waziri na Sumaye alikuwa Waziri mkuu, Nikachaguliwa tena Sumaye alikuwa waziri mkuu na Msekwa alikuwa Spika. Bilal alikuwa makamu wa rais nilifanya kazi na Pinda akiwa Waziri mkuu.
Na mimi natamani siku mmoja nistaafu niwe miongoni mwenu.
Nimepata nafasi ya kufanya kazi ya urais nikiwa na wazee wa kutosha. Nina marais wastaafu watatu. Katika Afrika ni nchi chache sana zenye bahati kama hii.
Nimepata nafasi ya kufanya kazi kukiwa na makamu wa rais, Mawaziri wakuu wastaafu kama Msuya, Salim, Msekwa, Sumaye, Lowassa, Pinda. Spika Wastaafu Wawili, Waziri wakuu wapo saba, Majaji wakuu watatu. Ni furaha sana.
Napenda kusikia kutoka kwenu twende uelekeo upi. Ntawaeleza nliyoyatekeleza na niayoyafanya hadi hapa tulipofikia na ninyi mtasema yapi mngependa yafanyike.
Naamini mazungumzo yetu ya kawaida kabisa yanaweza kutusaidia sisi wadogo zenu na vijana wenu tukawa na mengi ya kuzungumza na sisi tukawaeleza tunayoyafanya. Hilo ndio dhumuni kubwa.
Tanzania hii ni moja tunapeana vijiti anatoka huyu anaingia mwingine. Naomba mjisikie mpo nyumbani. Najisikia nipo na wazee wangu nategemea kujifunza kutoka kwenu. Wazee wangu karibuni sana.
Nmejisikia raha wazee nmewaita mnakuja japo sijawambia sababu ya kuwaita. Nakahisi hamtakuja lakini nashukuru kwa kuacha kazi zenu na kuamua kuja. Wengine siku nyingi sijawaona. Jaji Ramadhani sijakutana naye na Samatta sijakutana naye tangu astaafu. Sumaye tulikutana alipokuwa Hospital anaumwa sababu nlienda kumtembelea na Lowassa alikuja kunitembelea hapa Ikulu.
Nmefurahi kuwaona mkiwa na afya njema. Karibuni sana tuzungumze.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu Kiiongozi Balozi John Kijazi akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam ili kukutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wakuu na viongozi wastaafu ambao anakutana nao kwa mara ya kwanza wote kwa pamoja.
Viongozi Wakuu wastaafu wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam tayari kukutana na kuzungumza na mwenyeji wao Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyewaalika.
Viongozi Wakuu wastaafu wakimsikiliza Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza nao leo.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilali.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mtaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Waziri Mkuu Mstaafu, John Samuel Malecela.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Spika Mstaafu, Pius Msekwa.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Spika Mstaafu, Anne Makinda.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Jaji Mkuu Mstaafu, Jaji Barnabas Samatta.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Jaji Mkuu Mstaafu, Jaji Augustino Ramadhan.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Jaji Mkuu Mstaafu, Othman Chande
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Waziri Mkuu Mstaafu, Salim Ahmed Salim.
Social Plugin