Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAKUU WA MIKOA YOTE KESHO KUHUDHURIA TUKIO LA VIONGOZI WALIOTEULIWA NA RAIS MAGUFULI WAKIAPISHWA

Rais John Magufuli Jumatano Agosti 1, 2018 atawaapisha viongozi mbalimbali aliowateua Jumamosi iliyopita.


Taarifa iliyotolewa jana Julai 30, 2018 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imesema viongozi hao ni, wakuu wa mikoa wanne na makatibu wakuu wawili.


Wengine ni, naibu makatibu wakuu wawili na makatibu tawala wa mikoa 13.


“Wakuu wa mikoa yote ya Tanzania Bara mnapaswa kuhudhuria tukio hili,” imeeleza taarifa hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com