JamiiForums: Tumerejea baada ya kutoweka hewani kwa wiki 3
Wakuu,
Tumerejea hewani baada ya siku 21 tukiwa hatutoi huduma hii.
Kilichotokea:
Mnamo Jumapili, tarehe 10 Juni 2018 tulipata kuiona notisi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) ikitutaka kusitisha huduma mara moja nasi tulitii na kusitisha siku hiyo.
Tuliwasiliana na Mamlaka na ilitusikiliza na tukafuata taratibu za kujisajili ambapo wikiendi hii imetupa leseni ya miaka 3 na kuturuhusu kuendelea na huduma kwa wateja wetu.
Pamoja na mengine, tuliwasilisha maoni yetu kwa maandishi kwa mamlaka(TCRA) juu ya vipengele vya kanuni tunavyoona hazitekelezeki na kutoa mapendekezo ya maboresho. Tulisisitiza mambo manne kwa haraka:
1) Kanuni ya 5 kipengele (e) kinavunja haki ya faragha ya watanzania iliyowekwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi na utekelezaji wake utakuwa changamoto kwa wengi.
2) Kanuni ya 10 kipengele (b) inayolifanya kosa la jinai kutoweka nywila(password) kwenye kifaa cha kidijitali, tulishauri iangaliwe upya.
3) Kanuni ya 6 kipengele (3) inayotoa muda wa saa 12 kuondolewa kwa maudhui yanayolalamikiwa tulishauri iangaliwe upya kwani kwa uzoefu wetu inazuia haki ya kusikilizwa na kupelekea kuzimwa sauti za wananchi.
4) Gharama za usajili zilizowekwa zinazuia baadhi ya wanaotoa huduma kuendelea kufanya hivyo kwani si wote wenye uwezo huo na si kila blog inafanya kazi kibiashara. Tulipendekeza ikibidi yawekwe madaraja ili hata wale wadogo wasiachwe nyuma.
Mwisho:
Tunasikitika kwa kilichotokea hivyo tunaomba radhi kwa watumiaji kwa usumbufu wowote uliotokana na kusitishwa kwa huduma hii. Pia tunawashukuru kwa uvumilivu wenu na kuendelea kuwa nasi katika kipindi chote huduma ikiwa haipatikani.
Wateja wetu walio nje ya mipaka ya Tanzania walioathirika na yaliyotokea, tunawaomba radhi sana.
Asante

SOMA ZAIDI HAPA>>https://www.jamiiforums.com/threads/jamiiforums-tumerejea-baada-ya-kutoweka-hewani-kwa-wiki-3.1452491/
Social Plugin