KAMBI MAALUMU YA UCHUNGUZI NA TIBA YA MAGONJWA KUFANYIKA SHINYANGA..WANANCHI KUPATA HUDUMA BURE


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu kambi maalumu ya uchunguzi na tiba ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza itakayofanyika kuanzia Julai 17,2018 hadi Julai 21,2018 mjini Shinyanga- Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack ametangaza kufanyika kwa kambi maalumu ya uchunguzi na tiba ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza itakayofanyika kuanzia Julai 17,2018 hadi Julai 21,2018 katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga.


Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo,Jumatatu Julai 2,2018,Telack amesema kambi hiyo maalum ina lengo la kutoa huduma ya upimaji bure wa magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza.

Alisema kambi hiyo itakayodumu kwa muda wa siku tano itaendeshwa na madaktari bingwa kutoka ndani ya mkoa na wengine kutoka Hospitali za Bugando,KCMC,Hospitali ya taifa Muhimbili,Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na St. Thomas Arusha.

“Madaktari bingwa watatoa huduma katika fani mbalimbali ikiwemo upasuaji wa magonjwa ya ndani,mfumo wa mkojo ‘urology’,tezi dume,magonjwa ya akina mama na watoto,magonjwa ya ngozi,magonjwa ya mfumo wa macho,koo,masikio na pua pamoja na homa ya ini”,alieleza Telack.

“Wananchi watapatiwa huduma ya uchunguzi wa afya na kupewa huduma stahili za tiba na upasuaji kwa wananchi watakaothibitika kitaalamu”,aliongeza.

Aidha alibainisha kuwa wananchi zaidi ya 20,000 wanatarajiwa kufikiwa na kunufaika na huduma hiyo huku akiwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi hilo ili kupata huduma zitakazotolewa.

“Huduma zote za uchunguzi zitafanyika bila malipo,wenye kadi za bima za NHIF,CHF na nyinginezo watahudumiwa kwa kutumia kadi zao”,alieleza Telack.

ANGALIA PICHA
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu kambi maalumu ya uchunguzi na tiba ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza itakayofanyika kuanzia Julai 17,2018 hadi Julai 21, 2018 katika viwanja vya Shycom Manispaa ya Shinyanga - Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Waandishi wa habari wakichukua matukio wakati Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu kambi maalumu ya uchunguzi na tiba ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza
Waandishi wa habari wakiwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akisisitiza jambo
Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume akisisitiza umuhimu wa wananchi kujitokeza katika zoezi hilo ili kujua hali ya afya zao ikiwemo kupima ugonjwa hatari wa homa ya ini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post