Makao makuu ya Yanga
Katika mwendelezo wa sintofahamu inayoendelea kwenye klabu ya Yanga huku kukiwa na wimbi la viongozi wa ngazi mbalimabli kujiuzulu, aliyekuwa kaimu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga naye amejiuzulu nafasi yake.
Sanga amewasilisha barua kwa uongozi wa timu hiyo akiomba kujiuzulu nafasi ya Kaimu Mwenyekiti aliyoitumikia tangu mwaka 2017 alipojiuzulu aliyekuwa mwenyekiti Yusuf Manji. Pia amejiuzulu na nafasi yake ya msingi ya Makamu Mwenyekiti ambayo ndiyo ilimpa nafasi ya kuwa Kaimu Mwenyekiti.
Sanga ameitaja sababu kubwa iliyopelekea kuchukua uamzi huo ni kutokana na video iliyosambaa mitandaoni hivi karibuni ikionesha mashabiki wakihamasishana kwenda na mapanga kumfanyia fujo nyumbani kwake.
Kiongozi huyo sasa anafuata nyayo za viongozi wengine waliojiuzulu akiwemo aliyekuwa katibu mkuu Boniface Mkwasa, Mwenyekiti wa kamati ya kuinusuru Yanga Abbas Tarimba pamoja na wajumbe mbalimbali wa kamati ya utendaji ambao wameshachia ngazi.
Clement Sanga
Wakati hayo yanaendelea hali bado tete kwa upande wa wachezaji ambao wameripotiwa kugomea mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa marudiano ya kombe la shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia ya Kenya utakaopigwa kwenye uwanja wa taifa Julai 29, 2018.