Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KIMBUNGA CHAWASHUKIA WEZI WA MAJI JIJINI DAR ES SALAAM


Zoezi maalum la kubaini kaya zilizojiunganishia huduma ya Maji kinyume na utaratibu katika eneo la Mbezi Goigi na kufanikiwa kubaini wizi mkubwa wa Maji unaofanywa na baadhi wakazi katika kaya hizo.
Upekuzi ukiendelea ambao uliweza kubaini mashine zinazotumika kuiba maji.
Moja ya magari ambayo yalikuwa wakiuziwa maji.
Usalama ukiwa unasimamiwa kwa kiwango cha juu.

Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (Dawasco), limeendelea na zoezi maalum yakuibua wezi wa Maji katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam nakuwachukulia hatua kali za kisheria pamoja na kutaifisha vifaa vyote vinavyotumika wizi huo. 

Hayo yamebainshwa na Meneja wa Dawasco Mkoa wa Kawe Mhandisi Boniface Philemon wakati wa zoezi maalum linaloendeshwa na shirika hilo la kubaini kaya zilizojiunganishia huduma ya Maji kinyume na utaratibu katika eneo la Mbezi Goigi na kufanikiwa kubaini wizi mkubwa wa Maji unaofanywa na baadhi wakazi katika kaya hizo. 

“Tupo katika zoezi maalum la kubaini wizi wa Maji katika eneo hili la Mbezi Goigi na leo tumeweza kubaini wizi wa Maji katika kaya hizi mbili zilizofanya mchezo wakuharibu mita kwa kuondoa seal katika mita nakufanya mita hizo kutokuwa na uwezo wakufanya kazi kwa ufanisi”, alisema Mhandisi Boniface.

Hata hivyo Mhandisi Boniface ameendelea kueleza kuwa katika kaya hizo mbili wameweza pia kubaini visima vikubwa viwili vya Maji vyenye ujazo wa zaidi ya lita elfu 30,000 pamoja na Pampu kubwa sita zinazotumika kuvuta Maji na kuuzia wafanyabiashara wa magari ya Maji maarufu kama maboza wakati wa asubuhi na jioni ambapo ni kinyume na utaratibu wa Dawasco.

Kwa upande wa mjumbe wa eneo la Mbezi Juu Bi. Happiness Tarimo amekiri kuwa amekuwa akiona magari ya Maji yakiingia katika nyumba hizo na kutoka bila kuelewa kinachoendelea hivyo amewataka wakazi wa eneo hilo kutojihusisha kabisa na wizi wa Maji kwani ni kosa kisheria na atakaye bainika atachukuliwa hatua mara moja.

“Nimekuwa nikiona Magari ya Maji yakiingia na kutoka katika nyumba hizi mbili mara kwa mara bila kuelewa kama kuna jambo lolote linaloendelea ila nitoe wito kwa wananchi wangu tuepukane kabisa na wizi wa Maji maana ni sawa naku hujumu uchumi ukibainika tutakuchukulia hatua za kisheria” alisema Bi. Tarimo. 

Dawasco baada yakubainisha wizi huo wamechukua ya hatua kutaifisha pampu, mota zilizokuwa zinatumika kuchepushia Maji hayo pamoja na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria mmoja wa miliki wa nyumba hizo ambaye alikutwa katika eneo hilo wakati wa zoezi hilo maalum.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com