Lori limegonga daladala hiace tatu eneo la Mlima Mbalizi wilayani Mbeya na kuua watu 20 na kujeruhi wengine zaidi ya 40.
Ajali hiyo imetokea mchana wa leo Jumapili Julai Mosi, 2018 baada ya lori hilo kugonga daladala zilizokuwa zinatoka stendi ya Mbalizi kuelekea Mbeya mjini.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla na kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Mussa Taibu wapo eneo la tukio.
Kazi ya uokoaji inaendelea kufanywa na vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakishirikiana na wananchi kwani kuna watu bado wamelaliwa na magari.
Social Plugin