Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

LUGOLA AMTAKA ZITTO KABWE AJISALIMISHE.....MWENYEWE AGOMA AKIOMBA MBWA KWANZA

Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amemtaka mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe kujisalimisha kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi kwa maelezo kuwa ametoa kauli za uchochezi.


Lugola ametoa kauli hiyo leo Jumanne Julai 31, 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Amesema Zitto ametoa kauli za uchochezi na kuwatukana viongozi wa Serikali wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika jimbo la Kilwa Kusini.

Katika mkutano huo Zitto alialikwa na mbunge wa jimbo hilo, Seleman Bungara maarufu Bwege.

Hata hivyo Zitto Kabwe amekataa wito huo na kudai kuwa Waziri hana hayo mamlaka.

Waziri hana hayo mamlaka. Kama polisi wananitaka watoe wito wa kisheria nitakwenda. Naendelea na kampeni za Mbunge wa Buyungu ambapo tunamwunga Mgombea wa na madiwani wa kwenye kata kadhaa. Nashauri Waziri ampate kwanza yule Mbwa wa Polisi Bandari

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com