Ombi la pendekezo la mabadiliko ya vifungu vya katiba vya kumtaka
Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte kugombea tena Urais kwa awamu ya pili
limegonga mwamba na badala yake hataruhusiwa kugombea tena Urais muhula
wa pili.
Mabadiliko
hayo yaliyotangazwa na Jaji Mkuu Mstaafu wa Taifa hilo, Reynato Puno
Jumatatu ya Julai 16, 2018 yamemzuia Duterte kugombea Urais kwa muhula
wa pili huku baadhi ya vifungu vikimpa ahuweni Rais huyo mwenye maneno
makali kwa wakristo.
Hata
hivyo, duru za habari nchi Ufilipino zinasema kuwa Rais Duterte
hajastushwa na taarifa hizo na Chama chake kimesema kitafanya kila
liwezekanalo kiongozi huyo kugombea tena urais mwaka 2022.
Taarifa
hizo za Duterte kuonesha nia ya kutaka kuongoza tena kwa muhula wa pili
kwa nguvu zimepuuzwa na Rais Mstaafu wa taifa hilo, Aquilino “Nene”
Pimentel Jr. ambaye amesema kuwa anamfahamu na atamshauri Duterte
asing’ang’anie Madaraka na aheshimu katiba.
Mwezi uliopita Duterte aliwakasilisha wakristo nchini humo baada ya kunukuliwa akimdhihaki Mwenyezi Mungu kuwa ni ‘MPUMBAVU’.
Kwa
mujibu wa gazeti la GMA la nchini Ufilipino limeeleza kuwa Duterte na
Chama chake amepanga kujiuzulu urais miezi michache kabla ya Uchaguzi
Mkuu mwaka 2022 ili aweze kugombea tena kwani kikatiba inaruhusiwa.
Katiba
ya Ufilipino hairuhusu Rais wa nchi hiyo kugombea urais mihula miwili
mfululizo na Duterte analiongoza taifa hilo lenye Wakristo wapatao
milioni 88 hadi mwaka 2022.