MAFURIKO YAUA WATU 50


Moja ya sehemu iliyokumbwa na mafuriko nchini Japan

Watu 50 wamekadiriwa kupoteza maisha katika eneo la Hiroshima baada ya kutokea kwa mafuriko katika mfululizo wa mvua zinazoendelea kunyesha nchini humo.

Serikali imetoa tamko la watu wanaokadiriwa kuwa milioni mbili, kuhama makazi yao kwa sababu za kiusalama.

Mamlaka ya hali ya hewa imeripoti kuwa mvua zinazonyesha zitasababisha athari kubwa hasa eneo la mashariki mwa Japan

Miongoni mwa waliofariki ni pamoja na watu watano waliokandamizwa na mbao baada nyumba kuporomoka.

Msemaji wa mamlaka ya hali ya hewa nchini Japan ambaye ametambulika kwa jina moja Kyodo amesema kuwa jeshi la uhokoaji kwa kutumia ndege watazuru eneo la Okayama na Yamaguchi ambayo yameathirika zaidi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post