Rais Dkt. John Magufuli amesema kuwa anasikitishwa na baadhi ya viongozi wasiofanya maamuzi na badala yake majukumu yote wamemuachia Rais afanye hasa kuwajibisha wasiofanya vizuri kazini.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya uapishwaji wa viongozi aliowateua jana, ambapo amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri pamoja na makatibu wakuu.
“Viongozi wangu mmekuwa mkinisubiri kila kitu nifanye mimi tu, walioko chini yenu wanafanya vitu vya ajabu mnashindwa kuwawajibisha kila kitu mnasubiri maamuzi nifanye mimi”, amesema Rais Magufuli.
Na kuongeza kuwa , “Mfano, Mkoa wa Mbeya katika wiki mbili wamekufa watu 40, majeruhi zaidi ya 100, hakuna hatua zinazochukuliwa hata ya kuwambia RPC na RTO asijiuzulu. Au hadi wafe wangapi? mpunguzie hata nyota ili ajue damu za watu zinavyouma. Kaanze na RPC Mbeya”.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha Mawaziri watatu, makatibu wakuu pamoja na viongozi wengine wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) aliowateua siku ya jana alipofanya mabadiliko madogo katika safu ya Mawaziri.
Social Plugin