Josephine Matiro
Leo Jumamosi Julai 28,2018 Rais Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika nafasi
mbalimbali za kiuongozi wakiwemo wakuu wa wilaya,mikoa na makatibu
tawala.
Saa chache baada ya kuwepo
kwa taarifa za mabadiliko hayo,wananchi katika maeneo mbalimbali nchini
wamekuwa na mitazamo mbalimbali kuhusu wateule wapya lakini pia viongozi
walioondolewa katika nafasi walizokuwa wanazitumikia.
Katika Mabadiliko
hayo,miongoni mwa walioguswa ni Bi Josephine Matiro aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya
Shinyanga hadi leo Julai 28 ambaye nafasi yake imechukuliwa na Bi Jasinta
Venant ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo ya Shinyanga.
Kuachwa kwa Bi. Josephine
Matiro kumezua gumzo mitaani na hata kwenye mitandao ya kijamii watu wengi wamekuwa
wakiishia kusema ‘Ama kweli vizuri havidumu’.
Unaweza kusema,mabadiliko
yaliyofanywa na rais Magufuli yameleta kilio kwa baadhi ya wakazi wa Shinyanga
ambao wanasema,Matiro alikuwa kiongozi mchapakazi aliyependa wananchi bila
kujali hali zao.
Malunde1 blog imepata baadhi ya maoni ya
wananchi ....soma hapa chini
➤Maumivu niliyoyapata
kuhusu Matiro,daah sijawahi kuumia hivyo…..Alikuwa DC mahiri haijawahi tokea
kwa Shinyanga….Alipenda kusimamia kwenye ukwel haki na usawa.
➤Alikuwa ni mama mchapakazi, mwenye hofu na Mungu!!!
➤Hatuna jinsi. MUNGU atie nguvu dada tulimpenda, tulimzoea
alitusaidia. Basi tu Mungu atampa mlango wa kutokea. Amen.
➤Huyu mama nilimpenda sana japo sipo huko ila nilikuwa naona
anavyopambana bega kwa bega
➤Kiukweli... Alikuwa mchapakazi sana... Vizuri havidumu...Ntammiss pia
➤Dah Matiro wetuuuu ukweli chama hakiishi
➤Yaani mkuu Josephina matiro nimesikitika Sana nikiangalia alivyo kuwa Duuu Sina usemi tusubirie mengine haya yameshapita 😞
➤Yaani mkuu Josephina matiro nimesikitika Sana nikiangalia alivyo kuwa Duuu Sina usemi tusubirie mengine haya yameshapita 😞
➤Kasema watapangiwa kazi nyingine subirini uteuzi atakao
teuliwa
➤Mi binafsi nimeumia kwakweli jamani
➤Vizuri ndugu huwa havidumu sijui kwa nini? Tumwachie MUNGU.
➤Wachapakazi huwa hawakai sijui ni kitu gani,tulipata Matiro na Malecela lakini ndio hivyo!!🙏🙏🙏Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa Kila jambo
➤Kweli wazuri hawadumu ingawa uongozi ni kupokezana kijiti mkuu wetu wa wilaya shinyanga ameondolewa wakati tulikuwa tukimhitaji alikuwa mtu wa watu mpambanaji na msimamia ukweli ila tunaamini mungu atamfungulia mlango mwingine

➤But... I have faith...God has prepared something greater for her...
BOFYA <<HAPA>> KUANGALIA MATUKIO YALIYOFANYWA NA DC JOSEPHINE MATIRO SHINYANGA
BOFYA <<HAPA>> KUANGALIA MATUKIO YALIYOFANYWA NA DC JOSEPHINE MATIRO SHINYANGA
Social Plugin