Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MECHI ZA MCHUJO RAUNDI YA PILI JUMAPILI JULAI 1 - KOMBE LA DUNIA 2018


Mechi ya Kwanza:

Mwenyeji Urusi atakuwa nyumbani dhidi ya Mabingwa wa Dunia 2010 Uhispania.

Kipute kitagaragazwa uwanja wa Luzhniki, Moscow.

Mechi ya Pili:

Macho ya Watanzania na waafrika yatakuwa ugani Nizhny Novgorod wakati kijana wa 'Tanga' Yussuf Poulsen mwenye asili ya Tanzania, atakuwa anapiga kikosi cha Denmark dhidi ya Croatia.

Anatarajiwa kurejea baada ya kutumikia adhabu ya mechi moja nje kutokana na kadi mbili za njano alizokusanya Urusi.

Uwanja huo sio mgeni kwa Luka Modric na Croatia kwani mji Nizhny Novgorod ndio mji ulioandaa mechi ambayo Croatia iliidunisha Argentina 3 mtungi mbele ya Maradona mechi ya makundi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com