Mechi za robo fainali: Uruguay V Ufaransa, Brazil V Ubelgiji.
Kitakachovutia zaidi ni kuwa mastaa wa kizazi hiki, watakuwa wanawania umaarufu ndani ya siku hiyo kwa kuoneshana ubabe.
Luis Suarez wa Uruguay na Kylian Mbappe wa Ufaransa watakwatuana uwanja wa Nizhny Novgorod ulioko Nizhny Novgorod katika mechi ya kwanza.
Suarez, nyota wa Barcelona, amesajili mabao mawili hadi sasa naye Mbappe akiifungia Ufaransa mabao matatu yakiwemo yaliyomtoa Messi kwenye Kombe hili.
Hapo baadaye Neymar wa Brazil na Eden Hazard wa Ubelgiji watatoana jasho ugani Kazan.
Hata hivyo macho yote kwenye kikosi cha Ubelgiji kitakuwa kwa Romelu Lukaku anayeshikilia nafasi ya pili orodha ya wafungaji Kombe la Dunia hadi sasa.
Yote Tisa: Kumi, mastaa wawili watakaofanya vyema ndio watakaokutana nusu fainali na kurefusha muda wa kutawala vyombo vya habari na vinywa vya watangazaji na mashabiki!