MWIGULU NCHEMBA ATUA KWA KISHINDO JIMBONI KWAKE...AFUNGUKA KUHUSU RAIS MAGUFULI

Mbunge wa Iramba Magharibi,  Dk Mwigulu Nchemba amewataka wananchi wa jimbo hilo kutosikiliza maneno ya watu wanaosema kuwa anaweza kujiuzulu nafasi ya ubunge baada ya kuondolewa katika baraza la mawaziri.


Dk. Mwigulu ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Julai 7,2018 wakati akiwa kwenye mkutano na wakazi Kata ya Ulemo kijiji cha Misigiri wilayani Iramba mkoani Singida.

Amesema uongozi ni kupokezana kijiti na kwamba si kweli kwamba ana lengo la kuacha nafasi hiyo na kwamba ataendelea kuwatumikia wananchi wa jimbo lake kwa mda wote tofauti na mwanzo alivyokuwa kwenye majukumu ya kitaifa.

Ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais John Magufuli kwa kumwamini na kumpa na nafasi katika serikali yake hadi alipombadilisha na hana kinyongo chochote,  ataendelea kufanya kazi chini ya mwenyekiti wa CCM na serikali pale itakapoitajika huduma yake.  

"Sina kinyongo na Rais Magufuli, uongozi ni kupokezana kijiti",amesema Nchemba.

Amefafanua kuwa "uliona wapi mchezaji akasajiliwa kwenye klabu yake, kisha akaitwa timu ya taifa na siku akiondoka timu ya taifa anasema klabu yenu siichezei".

“Hao wanaosema nataka kujiuzulu ubunge, wanataka kutengeneza jambo la ugomvi. lakini kwangu sioni kama ni ugomvi wala tatizo nimerudi kuwatumikia wananchi wa jimbo kwa kazi mlionituma",ameongeza.

Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. John Pombe Magufuli alimteua Kangi Lugola kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nafasi ambayo ilikuwa inatumikiwa na Dk. Mwigulu Nchemba.

Mbunge wa Iramba Magharibi,  Dk Mwigulu Nchemba akiwahutubia wananchi wa Iramba



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post