POLISI DODOMA YANASA WEZI WANAOINGIA KWENYE MADUKA KWA PIKIPIKI

Jeshi la Polisi limewakamata watu wawili wanaotuhumiwa kuiba fedha kwa njia ya Mtandao, ambao wanatumia pikipiki yenye namba za usajili bandia MC. 759 AHW na Chassis namba PFZWFK47770 aina ya boxer.


Kamanda aliwataja Watuhumiwa hao kuwa ni Joseph Bakari Msinati (32) Mkazi wa Frelimo Iringa na Elisha Athman Mdemu(35)Mkazi wa Kihesa Iringa,ambao walitumia pikipiki hiyo kusafiri mikoa Mbalimbali mijini na vijijini kuiba bidhaa za dukani .


“Watuhumiwa hawa wanafika kwenye maduka na kuagiza bidhaa mbalimbali na kufanya malipo kwa njia ya mtandao wa simu, Mara baada ya kulipa na mpokeaji kujiridhisha kupokea fedha hiyo wanaondoka na bidhaa.


“Na baada ya dakika chache waharifu hao wanapiga simu kwenye Kampuni namba ya huduma kwa mteja na kudai kuwa warejeshewe fedha kwa kuwa wameituma kimakosa, na bidhaa kwenda kuuzwa kwa watu wengine kwa bei nafuu,” alisema Muroto.


Pia Kamanda alisema wamefanikiwa kumkamata Daudi Charles (25) Mkazi wa Mbagala akiwa na noti bandia 50 za shilingi elfu 10 ambazo zingekuwa halali thamani yake ni TSH. 500,000/=. 


Hata hivyo katika tukio lingine Kamanda alisema wamekamata mali mbalimbali za Wizi zilizotokana na matukio ya Uvunjaji na uporaji ambazo ni Televisioni 3,Magodoro 4,Redio Subwoofer 3,Majiko ya gesi 2,Spika 3,Deck 3,mifuko ya Cement 5 pamoja na Capeti 1.


Kamanda Muroto amewataka wananchi walioibiwa kufika polisi ili kuweza kuzitambua mali zao, Pia aliwatahadharisha Waharifu kuwa Dodoma siyo mahali Salama pa kufanyia uharifu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post