Rais John Pombe Magufuli (katikati) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya sh bilioni tisa ikiwa ni sehemu ya
gawio la sh bilioni 18 ambalo kampuni hiyo imetoa kwa wanahisa wake ambao ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
pamoja na Puma Investments Limited wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dr Phillip Mpango (kushotokwake), Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo Bw Prof Joseph Buchweshaija(kushoto) na Meneja Uendeshaji wa
Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania Bw Lameck Hiliyai(kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh bilioni tisa kwa Rais John Pombe Magufuli (katikati) ikiwa ni
sehemu ya gawio la sh bilioni 18 ambalo kampuni hiyo imetoa kwa wanahisa wake ambao ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Puma Investments Limited. Hafla
hiyo fupi imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dr Phillip Mpango
(wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo Bw Prof Joseph Buchweshaija.
*****
Kampuni ya mafuta ya Puma Energy Tanzania Limited imetangaza gawio la Sh.bilioni 18 kwa mwaka wa fedha wa 2017 kwa wanahisa wake.
Puma Energy Tanzania ni kampuni ambayo inayomilikiwa kwa pamoja na Serikali(kupitia Msajili wa Hazina, Wizara ya Fedha) pamoja na Puma Investments Limited, kila moja ikiwa na umiliki wa hisa kwa asilimia 50 imetanza gawio hilo leo jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti, ni kwamba ni kampuni ya mkondo wa kati kimataifa katika masula ya mafuta na pia kampuni ya mafuta inayojihusisha na uhifadhi mkubwa na usambazaji.
Amesema majukumu ya makuu ya kampuni ni masoko na usambazaji wa bidhaa za petroli ndani ya Tanzania. "Kampuni inauwezo wa kuhifadhi jumla ya lita za mafuta 94 milion, vituo 52 vya mafuta maeneo mbalimbali nchini na inahudumia viwanja vinane vya ndege. "Kufikia mwisho wa mwaka ulioishia 31 Desemba 31 2017 kampuni ilitengeneza faida kabla ya kodi ya jumla ya Sh. bilioni 31,"amesema.
Amefafanua kampuni iliwekeza takribani Sh.bilioni 9 bilioni kwa mwaka 2017 kununua na kuendeleza miundombinu ikiwemo kununua vituo viwili vya mafuta kwenye Jiji la Dodoma ikiwa ni juhudi za kuiunga Serikali mkono katika kuhamia Dodoma.Ameongeza wakurugenzi wa kampuni hiyo wamependekeza gawio la Sh.bilioni 18 kwa mwaka ulioishia Disemba 2017.
Ameongeza kila mwanahisa atapata Sh.bilioni 9 na kwamba mwaka 2016 Gawio lilikua Sh.bilioni 14 na 2015 gawio lilikua Sh.bilioni 9 .) "Kutokana na utendaji mzuri wa kampuni ya Puma Energy, gawio limekua kwa asilimia 100 ikilinganishwa na gawio la mwaka 2015 na kwa asilimia 29 ikilinganishwa na gawio na mwaka 2016.
"Ukuaji huu unaendana sambamba na mikakati ya kampuni ya kuhakiksha kampuni inaendelea kukua, kutengeneza faida, kukuza ajira nchini, kuchangia pato la taifa kupitia kodi, na kuendelea kuiunga serekali mkono katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo,"amesema Corsaletti.
Amesisitiza kuwa “Ufanisi wa kibiashara wa Puma Energy Tanzania kwa mwaka 2017 ulikua mzuri kwa pande zote za mauzo pamoja na mapato.
"Ufanisi wetu mkubwa unatokana zaidi na biashara ya mafuta ya ndege ambako kwa sasa sisi ndio tunaongoza katika soko,"amesema.
Meneja Mkuu huyo pia ameongeza kwa kueleza taaarifa za masoko zilizochapishwa na Mamlaka ya udhibiti (EWURA) inaonesha kuwa uwepo wa Puma Energy kwenye soko la mafuta umeongezeka kutoka asilimia 12 mwaka 2015 hadi asilimia 14 kwa mwaka 2017
Kwa kuongezea Corsaletti pia amepongeza juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli na Serikali yake katika mikakati yake ya kukusanya kodi na kutoa fursa kwa wawekezaji wa nje na ndani kama ilivyooneshwa kwenye bajeti ya 2017/2018.
"Mikakati hii imeweza kutengeneza mazingira rafiki kwa wawekezaji na kufanya makampuni mengi ikiwemo Puma kutengeneza faida zaidi,"amesema. Amefafanua mazingira hayo mazuri ya biashara yameiwezesha kampuni ya Puma kukua zaidi kutoa gawio mara mbili zaidi ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita.
Pia Puma itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na Serikali ya Awamu ya tano, na kuendelea kuchangia katika maendeleo ya taifa, hivyo uongozi wa Puma Energy utaendelea kutoa ushrikiano kama ambavyo wamekua wakishirikiana siku zote.Hivyo Puma imekabidhi gawio hilo leo kwa Rais Dk.John Magufuli ambapo pia kulikuwa na kampuni na mashirika mbalimbali yamekabidhi gawio kwa Serikali.