RAIS MAGUFULI KESHO KUONGOZA WATANZANIA KUPOKEA NDEGE

Ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 NextGen iliyowasili mwaka 2016

Watanzania wanatarajiwa kupokea ndege kubwa aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ilionunuliwa na serikali ya taifa hilo.


Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli atawaongoza raia wa taifa hilo katika sherehe ya mapokezi ya ndege hiyo.

Ndege hiyo inatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam majira ya saa nane mchana kutoka mjini Seattle Marekani.

Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari iliochapishwa na Mkurugenzi wa mawasiliano katika Ikulu ya rais, ndege hiyo ni ya nne kuwasili nchini humo kati ya saba zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kuliwezesha Shirika la Ndege la Tanzania {ATCL} kuimarisha huduma zake.


Ndege hiyo ina uwezo kubeba abiria 262.

Ndege nyingine ambazo zilinunuliwa na serikali ya Tanzania ni ndege moja aina ya Bombardier Q400 Dash 8 NextGen , ndege 2 aina ya Bombardier CS300 zenye uwezo wa kuchukua kati ya abiria 137 na 150 .

Mwaka 2016 Tanzania ilipokea ndege mpya ya kutumiwa na Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) katika hatua ya kuimarisha safari za ndani ya nchi za shirika hilo.

Ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 NextGen ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam (JNIA) kutoka Canada ilikotengenezewa.

Rais Magufuli alikuwa ameahidi kwamba shirika hilo lingeimarishwa na ndege mpya kununuliwa mara baada ya kuingia madarakani.

Baadhi ya maeneo ambayo ATCL inatarajia kuongeza safari zake ni Dodoma, Mwanza, Arusha, Mbeya, Kigoma, Tabora, Mpanda, Kilimanjaro, Mtwara, Zanzibar, Pemba, Bukoba na Visiwa vya Comoro.

Kulingana na Boeing, 787 Dreamliner ni familia yenye teknolojia ya kisasa ,ndege zenye utendaji mzuri na vitu vipya vya kupendeza.

Mbali na kuleta vigezo vya ndege kubwa katika ndege za wastani, 787 Dreamliner italipatia shirika la ndege la Air Tanzania ufanisi wa mafuta na mazingira ya utendaji, kwa kutumia chini ya asilimia 20 hadi 25 ya mafuta na asilimia 20 hadi 25 wa uchafuzi wa mazingira ikilinganishwa ndege nyengine zilizotumika awali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post