Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amefanya uteuzi wa mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), pamoja na makamishna watatu wa tume hiyo.
Rais Magufuli amefanya mabadiliko hayo leo, kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Balozi John Willium Kijazi, ambayo imesema kuwa Rais amemteua Athumani Kihamia kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kuchukua nafasi iliyoachwa na Ramadhani Kailima ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani.
Kabla ya uteauzi huo Kihamia alikuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, aidha Rais amefanya uteuzi pia wa makamishna wa tume ya uchaguzi, ambao ni Mbaruk Salim anayekuwa makamu mwenyekiti wa tume, Jaji mstaafu Thomas Mihayo na Balozi Omary Mapuli.
Balozi Kijazi amesema kuwa baada ya uteuzi wa viongozi hao, taarifa kuhusu tarehe ya kuapishwa itatolewa hivi karibuni.
.
Social Plugin