Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amewapongeza wanamichezo watatu walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kushika nyadhifa mbalimbali.
Wanamichezo waliopata nafasi hizo ni Mussa Ramadhan Sima aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Mazingira, Athuman Kihamia aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi katika Tume ya Uchaguzi (NEC) na Ramadhan Kailima aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Aidha, Rais Karia amesema kwa niaba ya TFF anawapongeza wanamichezo hao kwa nafasi zao mpya walizoteuliwa huku akidai anaamini kwa uchapakazi wao hawatamuangusha Rais Magufuli.
"Kwa niaba ya TFF nawapongeza wanamichezo wenzetu Kihamia ,Sima na Kailima kwa uteuzi wa nafasi zao mpya na nawatakia kila la heri kwenye nafasi zao", amesema Karia.
Kihamia yupo kwenye Kamati ya Ajira ya TFF wakati Sima ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira Wa Miguu Mkoa wa Singida.
Chanzo- EATV
Social Plugin