Klabu ya Mabingwa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wapo mbioni kufuata nyayo za watani wao wa jadi 'Yanga' kwa kutengeneza wimbo maalum utakao kuwa unawatambulisha wao katika michezo mbalimbali watakayokuwa wakishiriki.
Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na Msemaji wa Simba, Haji Manara leo (Julai 05, 2018) kupitia ukurawa wake wa kijamii na kupelekea mashabiki wa Msimbazi kupokea taarifa hizo kwa furaha tele zikiwa zimeambata na fursa za kufanyakazi.
"Ni nani au kikundi gani kitashinda kuimba wimbo rasmi wa Simba?. Ukishinda au wakishinda watapata fursa ya kurekodi na msanii mkubwa nchini 'official song' ya Simba na studio ya Lamaar", ameandika Manara.
Mbali na hilo, Manara amewaomba wanasimba, wadau wa soka pamoja na watu mbalimbali wenye vipaji vya kuimba wachangamkie fursa hiyo kwa kutuma 'sample' za wimbo walizoimba ili ziweze kupuitishwa na kuingia rasmi kwenye mchakato ambao wako mbioni wa kutengeneza wimbo wa klabu.
Ikumbukwe, Klabu ya Yanga ndio ya kwanza kuanza kutangaza nia hiyo ya kutaka kutengeneza wimbo wao maalum mnamo mwezi Machi 22, 2018 kupitia msemaji wao Dismas Ten lakini hadi hii leo hakuna wimbo wowote ulioweza kutangazwa licha ya kuonekana wapo studio za 'FishCrab' na 'Producer' BongoFleva Lamar ambaye kwa sasa Simba nao wamepanga kumtumia pia.