TAZAMA HAPA MAJINA YA WALIMU WA AJIRA MPYA WALIOPANGWA VITUO VYA KAZI JULAI, 2018

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJIRA YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI JULAI, 2018
Ofisi ya Rais – TAMISEMI inapenda kuutarifu Umma kuwa, jumla ya Walimu 4,840 wamepangiwa vituo vya kazi kwenye Shule mbalimbali za Msingi na baadhi kwenye Shule za Sekondari nchini. 

Walimu hao waliopangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kuripoti katika Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri zilipo shule walizopangiwa na baadaye kuripoti kwenye Shule walizopangiwa. 

Walimu wote wanatakiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi kuanzia tarehe 23 Julai, 2018 hadi tarehe 7 Agosti, 2018 wakiwa na mahitaji yafuatayo:
  • Vyeti halisi vya taaluma vya Kidato cha Nne na/au Kidato cha Sita;
  • Vyeti halisi vya kitaaluma vya mafunzo ya Ualimu katika ngazi husika; na
  • Cheti halisi cha kuzaliwa.
Walimu wote waliopangiwa vituo vya kazi wanaelekezwa kuwa:
  • Vituo vyao vya kazi ni Shule ya Msingi au Sekondari alizopangiwa na sio Makao Makuu ya Halmashauri;
  • Mwajiriwa atakayeripoti na kuchukua posho ya kujikimu kisha akaondoka katika kituo chake cha kazi alichopangiwa Serikali itamchukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo; na
  • Hakuna Mwalimu atakayekubaliwa kubadilisha kituo kwa sababu yoyote ile. Kila mwajiriwa mpya anapaswa kuripoti katika kituo chake alichopangiwa na si vinginevyo. Waajiriwa wapya ambao watashindwa kuripoti katika vituo walivyopangiwa nafasi zao zitachukuliwa na Walimu wengine 5,220 wenye sifa waliokosa nafasi.
Wakurugenzi wa Halmashauri husika wawapokee Walimu waliopangwa kwenye Halmashauri zao kwa kuzingatia taratibu na kanuni zote za utumishi wa Umma, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa ya kuripoti kwao. Taarifa ya kuripoti waajiriwa hao itumwe Ofisi ya Rais- TAMISEMI ifikapo au kabla ya tarehe 10.08.2018 baada ya tarehe ya mwisho ya kuripoti.
 
Majina ya Walimu waliopangiwa vituo yanapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz
 
Imetolewa na:
KATIBU MKUU OFISI YA RAIS – TAMISEMI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post