WALIOPEANA TALAKA WANAONGOZA KWA MAAMBUKIZI YA VVU

 Utafiti wa kitaifa wa viashiria na matokeo ya Ukimwi kwa mwaka 2016/17 unaonyesha wanandoa waliotalikiana wanaoongoza kwa asilimia 11 kuwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU).


Akizungumza leo Jumanne Julai 24, 2018 katika semina ya wahariri na utoaji wa matokeo hayo, mratibu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) Mkoa wa Tanga, Juma Billingi amesema wanandoa nao wanapata maambukizi ya VVU kwa asilimia 4.8.


“Hakuna sababu moja maalumu ya wanandoa au waliotalikiana kuwa na maambukizi kwa kiasi kikubwa kwani zipo sababu nyingi,”amesema.

“Kwa upande wa maambukizi mapya Watanzania 81,000 wanapata maambukizi mapya kila mwaka sawa na asilimia 9.2.”

Kadhalika amesema mkoa unaoongoza kwa maambukizi ni Njombe wenye asilimia 11.4 ukifuatiwa na Iringa asilimia 11.3 mkoa wa mwisho kwa maambukizi ni Lindi wenye asilimia 0.3.

Kitaifa, Bilingi amesema kwa sasa kiwango cha maambukizi nchini ni asilimia 4.7 ikilinganisha na asilimia 5.1 miaka minne iliyopita.
Na Taus Mbowe, Mwananchi 
SOMA ZAIDI HAPA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post