Kundi la wanakijiji limewaua takribani mamba 300 kwenye makao ya wamyama katika mkoa wa West Papua nchini Indonesia.
Mauaji hayo yalikuwa ni ya kulipiza kisasi kifo cha mwanamume mmoja ambaye aliuawa na mamba mmoja eneo hilo.
Maafisa na polisi wanasema kuwa hawakuweza kuzuia mauaji hayo lakini watafungua mashtaka dhidi ya waliohusika.
Kuuawa kwa wanyama wanaolindwa ni hatia na adhabu yake inaweza kuwa kifungo jela nchini Indonesia.
Mwanakijiji huyo aliuawa siku ya Ijumaa asubuhi wakati akitafuta mboga eneo la kuzalia mamba.
Mfanyakazi mmoja alisikia mtu akiitisha msaada na alipofika huko aliona mamba akimshambulia mtu.
Baada ya mazishi siku ya Jumapili, wanakijii mamia kadha wenye hasira walielekea eneo la makao ya wanyama wakiwa wamejihami kwa visu, chuma, nyundo na sururu.
Vyombo vya habari vinasema kuwa wanakijiji waliishambulia ofisi kwenye makao ya wanyama na kisha kuwachinja mamba wote 292.