Picha ya nyumba ambapo watu 11 wamepoteza maisha.
Watu 11 wa familia moja wamepatikana wakiwa wamekufa kwenye nyumba iliyo katika mji mkuu wa India Delhi, huku 10 kati yao wakiwa wananing'inia katika dari la nyumba hiyo, kwa mujibu wa polisi.
Mwanamke mmoja aliye na takribani miaka 70 alipatikana kwenye sakafu ya nyumba. Wengi wa wale waliokuwa wamekufa walikuwa wamefungwa macho na mikono nayo ilikuwa imefungwa kwa kamba mgongoni.
Familia hiyo imeishi wilaya ya Burari mjini Delhi kwa zaidi ya miaka 20 licha ya kwamba wametokea katika maeneo ya Rajathan huku familia hiyo ikiwa inamiliki maduka mawili katika ghorofa ya chini kwenye jengo la ghorofa tatu.
“Nilipokuwa naenda dukani niliona mlango ukiwa umefunguliwa na nilipoingia ndani niliona miili ya watu hao ikiwa imening’inia katika dari huku imefungwa mikono kwa nyuma” amesema Gurchan Sigh alipokuwa akihojiwa na moja ya chombo cha habari mjini Delhi.
Huku taarifa ya awali kutoka polisi inazungumzia karatasi zenye maandishi walizozipata kwenye nyumba hiyo ambazo zinaashiria kufanyika kwa matambiko yanayoonekana kuwa na uhusiano na vifo hivyo.
“Bado tunasubiri matokeo ya upasuaji, na kuwahoji majirani na kuchunguza video za CCTV eneo hilo” amesema afisa mmoja wa polisi alipokuwa akizungumza na chombo cha habari uko mjini Dehli..
Sababu za mauaji hayo pamoja na wahusika bado hazijawekwa wazi na polisi mjini Delhi imesema kutoa taarifa baada ya uchunguzi kufanyika.
Social Plugin