WAZIRI UMMY AWATAKA WADAU WA MAENDELEO SEKTA YA AFYA KUWEKEZA KWENYE MASUALA YANAYOGUSA WANANCHI

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewataka wadau wa maendeleo katika sekta ya afya kuwekeza nguvu katika masuala yanayowagusa wananchi moja kwa moja.

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati alipotembelea Kituo Cha Afya cha Ilagala kilichopo wilayani Uvinza mkoani Kigoma katika ziara yake ya kujua hali ya utoaji wa huduma za afya mkoani humo.

"Nataka kuona wadau wa maendeleo ya afya wanakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi hususan huduma za afya ya mama na mtoto kuliko kujikita kwwnye semina", alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amewapongeza wadau wa maendeleo katika sekta hiyo wakiwemo ENGENDER HEALTH na THAMINI UHAI kwa kujenga chumba cha upasuaji na kutoa Pikipiki za watumishi katika Kituo cha afya Ilagala na zahanati ya Kalenge wilayani Uvinza Mkoani Kigoma.

Mbali na hayo katika ziara hiyo Waziri Ummy amesema kuwa Serikali ya Rais John Pombe Magufuli kupitia Wizara yake haitaki kuona wananchi wanapata huduma duni za afya.

Waziri Ummy amesema kuwa katika kuhakikisha huduma bora za afya zinatolewa katika Wilaya ya Uvinza imetenga shilingi milioni 300 kwa ajili ya vifaa na vifaa tiba katika Kituo cha afya Uvinza pamoja na mashine ya kutoa huduma ya usingizi katika kituo cha Afya Ilagala kuhudumia vizuri wanaohitaji huduma ya upasuaji.

Alisema amewasisitiza wauguzi na watoa huduma za fya kwa ujumla kuwa na matumizi ya lugha nzuri kwa wananchi wanaowapa huduma katika vituo vyao vya kazi.

"Nasisitiza kwa muuguzi na mtoa huduma za afya yeyote atakayekutwa anatoa lugha chafu na haziridhishi kwa mwananchi hususan mgonjwa hatua kali zitachukuliwa mara moja ",alisema Waziri Ummy.

Na Editha Karlo- Malunde1 blog Kigoma
Waziri wa Afya, Maendelo ys Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akimsalimia Mama aliyejifungua Bi. Amina Joseph (23) mkazi wa Ilagala wakati alipotembelea kituo cha Afya Ilagala wialayani Uvinza mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kujua hali ya utoaji wa huduma za afya mkoani humo. Picha zote na Editha Karlo- Malunde1 blog Kigoma
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwajulia hali baadhi wananchi waliokuwa wanapata huduma katika kituo cha Afya Uvinza wakati wa ziara yake ya kuangalia upatikanaji wa huduma za afya katika mkoa wa Kigoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiangalia dawa zinazopatikana katika stoo ya dawa ya Zahanati ya Kalenga wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utiaji huduma za afya Mkoani Kigoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikagua ujenzi wa moja ya nyumba za watumishi katika Kituo cha Afya Uvinza wilayani Uvinza mkoani Kigoma wakati wa ziara ya kuangalia hali ya utoaji huduma za afya mkoani humo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post