Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MKUU AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI WATATU HOSPITALI YA KASULU MJI KWA TUHUMA ZA KUIBA DAWA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Bibi Pendo Lilola kwa kujifungua salama mtoto wa kiume katika wodi ya wazazi kwenye Hospitali ya wilaya ya Kasulu akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
***

Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa amewasimamisha watumishi watatu wa Hospitali ya Wilaya ya Kasulu Mji ambao wanatuhumiwa kuiba dawa na kwenda kuuza katika maduka ya mjini.

Aidha, Waziri Mkuu ameahidi kuyafunga maduka yote yanayo nunua dawa kwa Watumishi ambao wanaiba dawa katika hospitali za Wananchi na kwenda kuuza kwa ajili ya kujinufaisha wao.

Waziri Mkuu alifikia uamuzi huo leo wakati alipotembelea Hospitali ya Wilaya ya Kasulu na kuwepo na tatizo la upotevu wa dawa na vifaa tiba katika hospitali hiyo na kumuagiza mganga Mkuu kuwasimamisha kazi watumishi hao wapishe uchunguzi na watakapo bainika wanahusika na tuhuma hizo hatua kali zichukuliwe dhidi yao.

"Watumishi wazembe , wezi na wala rushwa na wasio waadilifu hawatufai katika serikali yetu na kamwe hatutawavumilia hivyo tutawaondoa",alisema.

Aliwataja watumishi wanao husika ni wanaohusika na tuhuma hiyo ni Michael Nindi ambaye ni mfamasia wa wilaya , Tilasi Mbombwe ambae ni mtu wa maabara na Venancea Batega muuguzi.

Na Rhoda Ezekiel Kigoma

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com