Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AJALI YAUA WATATU WA FAMILIA MOJA

Watu wanne wamefariki dunia watatu wakiwa ni wa familia katika ajali iliyohusisha gari na pikipiki.


Akizunguma na wanahabari jana Agosti 2, Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma Gilles Muroto, alisema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia jana wilayani Bahi, Dodoma kwenye barabara kuu ya Singida-Dodoma.


Waliofariki ni watoto Yusra Salum (5), Karialino Hamis (2), Hussein Hamisi (miezi miwili) na Mfaume Hamis (30) ambaye alikuwa dereva wa bodaboda.


Kamanda Muroto amesema mwendesha pikipiki huyo alikuwa amewapakia watoto watatu na mama yao na aliingia barabarani ghafla na pikipiki hiyo iligongwa na basi la kampuni ya Satco.


Muroto ameeleza kuwa basi hilo lilikuwa likitokea Mwanza kuelekea jijini Dar es salaam.


“Kwenye hiyo pikipiki walikuwa wamepanda jumla ya watu watano, watoto watatu na mama yao dereva amefariki dunia papo hapo na watoto watatu mama huyo na mama mwenyewe naye ni majeruhi hospitali,”alisema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com