Mbunge wa jimbo la Mtama Nape Nauye (CCM) amewataka wapinzani kubishana kwa hoja mambo gani waliyoyafanya katika jimbo la Buyungu na CCM waliyoyafanya kuwaletea miradi ya maendeleo wananchi wa Buyungu na sio kuwadanganya wananchi wa Buyungu.
Nauye amesema hayo leo katika kijiji cha Nyakayenzi kata ya Kasuga wilayani Kakonko wakati akimnadi mgombea wa chama hicho, ambapo alisema wapinzani wanatakiwa kubishana kwa hoja kwa kutangaza mazuri waliyoyafanya kwa kipindi cha miaka mitatu waliyoaminiwa na wananchi wa Buyungu ni miradi ipi walioileta na vitu walivyovifanya.
Amesema wapinzani wasipobadilika siasa wanazozifanya kwa sasa ,upinzani utafutika kwa kuwa wananchi wanaona kazi inayofanywa na serikali iliyoko madarakani na wasipobadiliku na kuacha kuisema vibaya watakimbiwa na viongozi wote na wanachama.
Amesema nje ya miradi iliyotekelezwa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi wakati wa utawala wa mgombea wa CHADEMA ambaye anagombea kiti hicho hakuna ambacho walikifanya na wanatakiwa kuacha kuwadanganya wananchi kwamba wao wamefanya kwa kuwa hawana serikali na serikali iliyopo madarakani ni ya CCM.
Ameeleza kuwa kwa kipindi ambacho Christopher Chiza amekuwa madarakani ameweza kuleta miradi ya kilimo cha mpunga katika skimu za umwagiliaji za Katengera na Ruhiti pamoja na umeme na miradi ya maji ambapo amewaomba wananchi wamchague Chiza aweze kuendeleza miradi ambaya haijakamilika.
Amesema Serikali inayotoa fedha za miradi ni ya CCM na vyama vya upinzani havina serikali hivyo wananchi wasidanganyike na wamchague mgombea wa chama hicho ili maendeleo yaweze kuletwa katika wilaya ya Kakonko.
"Vyama vya siasa vya upinzani wanafanya mchezo mchafu Upinzani huwa hawasemi kwamba hawana serikali ,wakati Chiza anapendekeza Kakonko iwe Wilaya kulikuwa hakuna sifa ya kuwa na wilaya kwa uwezo alionao Chiza aliweza kuleta wilaya ,tangu mumchague kiongozi wa upinzani hakuna kilichofanyika lazima Wanakakonko mbadilike", amesema Nauye.
Naye mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Christopher Chiza ameahidi kuwatumikia wananchi kwa kuwaletea maendeleo.
Amesema wakati akiwa mbunge aliomba shilingi Milioni 264 kwa ajili ya kujenga madarasa , na fedha hizo zimeletwa kutokana na ufuatiliaji wake na pia aliomba itolewe fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya na serikali imepitisha na mpaka sasa wametengewa bajeti ya shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi huo .
Amesema ili hospitali hiyo ikamilike zinahitajika zaidi ya bilioni sita na amewaomba wananchi wamchague ili aweze kwenda kupigania haki ya Wanakakonko na fedha hizo ili nao waweze kupataa huduma karibu.
Na Rhoda Ezekiel - Malunde1 blog Kigoma,
Mbunge wa jimbo la Mtama Nape Nauye (CCM) akimnadi mgombea ubunge jimbo la Buyungu Christopher Chizz
Na Rhoda Ezekiel - Malunde1 blog Kigoma,
Mbunge wa jimbo la Mtama Nape Nauye (CCM) akimnadi mgombea ubunge jimbo la Buyungu Christopher Chizz
Social Plugin