Siku moja mara baada ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mh. Jokate Mwegelo amefuta picha zote zilizokuwa katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.
Ukurasa huo wenye followers Milioni 3.1 kwa sasa unaonekana mweupe kabisa. Huu umekuwa ni mtindo wa mastaa wengi Bongo kufanya kitu kama hicho kwa sababu maalum, Wema Sepetu, Mwasiti, Ben Pol na wengineo walishafanya hivyo pia.
DC Jokate alirejea katika mtandao wa Instagram July 29, 2018 ikiwa ni siku moja tangu alipoteuliwa na Rais John Magufuli katika nafasi hiyo ya uongozi.
Kwa kipindi cha takribani miezi mitatu cha kuanzia April 20, 2018 hadi tarehe ya uteuzi alikuwa hajachapisha chochote katika mtandao huo.
Social Plugin