JWTZ YATANGAZA AJIRA KWA VIJANA

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza nafasi za kuandikishwa jeshini madaktari wa binadamu na fani nyingine za tiba.


Taarifa hiyo imetolewa jana tarehe 31, 2018 na Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano JWTZ, Kanali Ramadhan Dogoli wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.


“Nafasi hizo zinatolewa ili kuongeza idadi ya wataalamu wa tiba watakaotoa huduma za afya katika hospitali zetu, vituo vya afya na Zahanati kulingana na mahitaji ya sasa na siku zijazo,” alisema Kanali Dogoli.


Alisema watakao andikishwa Jeshini ni wale wenye taaluma za Doctor of Medicine, Doctor of dental sugery, bachelor of pharmacy, bachelor in laboratory science, bachelor of science in nursing, bachelor of science in physiotherapy na bachelor of science in prosthetics and orthotics.


Kanali Dogoli ametaja sifa za watu wanaohitajika kuandikishwa ikiwemo, mhusika awe na umri kati ya miaka 18 hadi 28 na mzaliwa wa Tanzania, awe hajawahi kupatikana na hatia ya makosa ya jinai mahakamani na kufungwa jela, awe na cheti halisi cha kuziliwa.


Pia, kama ni daktari awe amemaliza mafunzo kwa vitendo na kutunukiwa vyeti pamoja na kusajiliwa na Bodi. Awe hajawahi kutumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo.


Kanali Dogoli amesema wenye sifa tajwa na kuhitaji kujiunga na JWTZ waripoti katika kambi ya Jenerali Abdallah Twalipo, Mgulani Dar es Salaam tarehe 28 Agosti, 2018 kuanzia saa moja asubuhi.


“Watakaochaguliwa na kuandikishwa jeshini watapatiwa mafunzo mbalimbali ya jeshi na yatakayo waendeleza katika taaluma zao. Wakiwa Jeshini majukumu watakayopatiwa ni yale yatakayowapachangamoto na fursa nzuri za kutumia taaluma zao,” alisema Kanali Dogoli.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post