Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu (Kushoto) akimkabidhi ofisi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti leo Jumatatu Agosti 6,2018 - Picha na Editha Karlo - Malunde1 blog
Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewataka wanakagera kumpa ushirikiano katika majukumu yake mapya ya kikazi aliyoanza ili kuendeleza yale mazuri yaliyofanywa na watangulizi wake.
Gaguti ameyasema hayo leo kwenye ukumbi wa halmashauri ya Bukoba baada ya kukabidhiwa ofisi na Mkuu wa Mkoa mstaafu Meja Jenerali Salum Kijuu na kumuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu.
Alisema nafasi yake ni kuendeleza yale mazuri yaliyofanywa na watangulizi wake kwa wanakagera ili kuhakikisha Mkoa wa Kagera unasonga mbele.
"Ni wajibu wangu kuendeleza yale mazuri yaliyofanywa na watangulizi wangu na nina imani kubwa tutashirikiana na viongozi wenzangu na nitatoa ushirikiano wakati wowote nipo tayari"alisema Mkuu huyo wa Kagera
Gaguti alisema Mkoa wa Kagera ni Mkoa ambao upo mpakani na unapakana na nchi karibia tatu hivyo aliwataka wananchi wa Mkoa huo kutumia fursa hiyo kuuza mazao ili kuufanya Mkoa kuwa wa viwanda na wenye neema.
Mkuu wa Wilaya ya Kywerwa Rashid Mwaimu baada ya kuapishwa alisema kuwa atakwenda kusimamia mapato katika Wilaya yake na kuhakikisha yanaongezeka ili shuhuri za maendeleo ndani ya Wilaya hiyo zifanyike vizuri.
"Najua nina majukumu makubwa na kazi yangu ni kutatua matatizo ya wananchi ili Wilaya yetu iweze kufanya vizuri katika sekta za miundombinu,afya na elimu"alisema.
Na Editha Karlo - Malunde1 blog
Social Plugin