Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku ‘King Msukuma’ amemwakikishia mgombea udiwani wa chama cha Mapinduzi Nikodemus Bonifasi kuwa atashinda kwa kishindo katika uchaguzi wa Marudio utakaofanyika Agosti 12 mwaka huu.
Msukuma amemtabiria ushindi huo Mgombea huyo akiwa katika mkutano wa kampeni kata ya Bagara mjini Babati uliofanyika mtaa wa Osterbay na kuhudhuriwa na Mamia ya wakazi wa Babati.
Huku msukuma akitumia zaidi ya dakika 45 kumnadi mgombea huyo maarufu kwa jina la Nyeusi aliongoza maandamano ya amani hadi ofisi za Ccm mtaa wa Osterbay kwa miguu na kuziba bara bara kwa muda huku wakiimba na kucheza nyimbo maarufu ya chama hicho ‘Ccm mbele kwa mbele.
Uchaguzi huu katika kata ya Bagara unakuja baada ya diwani wa Chadema Bwana Nyeusi ambaye ndiye mgombea wa CCM kukihama cha hicho.
Kwa upande wa Chadema wamemsimamisha mwenyekiti wa mtaa wa Miomboni Mathayo Zebedayo kugombea nafasi hiyo.
Social Plugin