Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangala amefikishwa katika Hospitali ya Selian Lutheran Medical kwa ajili ya kupatiwa matibabu kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea leo asubuhi eneo Magugu Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara.
Baada ya kutua kwa Helikopta katika Hoteli ya Mount Meru, msafara ulienda moja kwa moja hospitali hiyo tofauti na ilivyotarajiwa kufikishwa Hospitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru.
Wakuu wa mikoa ya Arusha,Mrisho Gambo na Kilimanjaro, Anna Mgwira ,Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo pamoja viongozi wa Kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wapo katika hospitali hiyo.
Taarifa zaidi zinasema baada ya kupata huduma ya kupigwa picha atasafirishwa na ndege maalumu kwenda Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.
Gari la Waziri Kigwangalla limepata ajali leo asubuhi eneo la Magugu, Manyara. Ajali hiyo imesababisha kifo cha msemaji wa mizara hiyo, Hamza Themba.
Social Plugin