Kocha wa Man United Jose Mourinho leo amenukuliwa na vyombo vya habari akielezea namna ambavyo anakutana na changamoto ya kuwakosa baadhi ya mastaa wake katika kikosi chake wakati wa maandalizi ya msimu wakiwa mapumzikoni baada ya World Cup.
Man United walikuwa na jumla ya wachezaji 11 katika michuano ya World Cup ambao walikuwa wamegawanyika katika mataifa tofauti tofauti, kati ya hao wachezaji 7 ambao ni Marcus Rashford, Romelu Lukaku, Paul Pogba, Marouane Fellaini, Phil Jones, Ashley Young na Jesse Lingard wote timu zao zilishiriki hadi mwisho wa mashindano.
Hivyo mastaa hao wanatajwa kuwa wanaweza kukosa mechi za mwanzoni za Ligi Kuu England msimu wa 2018/19 lakini leo Jose Mourinho amethibitisha kuwa Lukaku, Rashford na Jones tayari wamerudi kuungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya game yao ya ufunguzi EPL dhidi ya Leicester City August 10 2018.
Social Plugin