Mwanafunzi wa darasa la kwanza mwenye umri wa miaka minane mkoani Manyara, anadaiwa kubakwa na mkazi mmoja wa wa Kijiji cha Maganjwa wilayani Babati na kumsababishia ugonjwa wa fistula.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Dareda, Joseph Lorri, alithibitisha kupokewa mtoto huyo ambaye alikuwa na hali mbaya ikiwamo kuvuja damu kutokana na majeraha ya kuchanika sehemu za siri ikiwamo haja ndogo na kubwa.
Alisema mtoto huyo alipokewa hospitalini hapo Julai 16, mwaka huu saa 3.30 usiku akiwa ameharibiwa sehemu zake za siri na anavuja damu na kutokwa nyama sehemu zake za siri.
“Tukio lenyewe linavyoelezea mtoto huyu alibakwa, na mtoto alimtaja aliyembaka ambako jamii ilikuwa ikimtafuta mbakaji huyo.
“Alivyoletwa alikuwa anatoka damu sehemu za siri na kulikuwa na mpasuko wa kidonda kwenye sehemu ya haja kubwa na ndipo tukaanza kumfanyia vipimo,” alisema Dk. Lorri.
Alisema mtoto huyo alitibiwa kwa kufanyiwa upasuaji na kushonwa kuunganisha sehemu hizo zilizochanika na kwamba hadi sasa hali yake inaendelea vizuri kwa uangalizi wa madaktari wa hospitali hiyo.
“Tunaendelea na jitihada za kumtibu lakini pi tumemwanzishia matibabu ya dawa za kumkinga dhidi ya maambukizi ya virusi kutokana na tukio lenyewe jinsi lilivyokuwa,” alisema
Social Plugin