Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (Rufaa), Semistocles Kaijage (katikati) akizungumza na baadhi ya Mafundi na Wahandisi wa Mradi wa Ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoka TBA na Chuo Kikuu Ardhi alipotembelea eneo la mradi wa ujenzi wa Ofisi hizo eneo la Njedengwa leo jijini Dodoma. Wengine ni Wajumbe na Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (Rufaa), Semistocles Kaijage (katikati) akikagua eneo linapojengwa ghala la kuhifadhia vifaa vya uchaguzi akiwa ameambatana Wahandisi wa Mradi wa Ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoka eneo la Njedengwa leo jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (Rufaa), Semistocles Kaijage (katikati) akizungumza na Wajumbe na Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (kulia) mara baada ya kutembelea eneo la mradi la ujenzi wa Ofisi za NEC jijini Dodoma. Wengine (kushoto) ni Mafundi na Wahandisi wa Mradi wa Ujenzi wa jengo hilo kutoka TBA na Chuo Kikuu Ardhi.
Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Muhandisi Geofrey Mushanyela akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa ofisi hizo kwa wajumbe na watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi waliotembelea mradi huo leo jijini Dodoma.
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakipita mbele ya jengo la Utawala la Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiongozwa na Wahandisi wanaosimamia mradi huo kutoka TBA na Chuo Kikuu Ardhi. Jengo hilo la Ofisi za NEC linajengwa eneo la Njedengwa jijini Dodoma leo. PICHA/ TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI