Dave Fawbert alimuona nyoka huyo huko Leytonstone, mapema Jumamosi.
Shirika linaloshughulika na wanyama RSPCA limemchukua nyoka huyo na linaomba habari kuhusu ni kwa njia gani alipata kufika eneo hilo.
Video ya nyoka akimla njiwa London yasambazwa sana mitandaoni
Bw Fawbert alisema kwa asilimia 100 nyoka alikuwa akimla njiwa huyo na kwamba tayari alikuwa amemla nusu.
Anasema alitaka kumuona nyoka akiwa safarini nchini Tanzania miaka michache iliyopita lakini hakufanikiwa, lakini sasa amemuona. alisema.
Video hiyo kwenye akaunti yake ya Twitter imesambazwa mara 4,000.
Wengine wanamtaja nyoka huyo kuwa chatu.
Chanzo-BBC
Social Plugin