Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa.
Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Zimbabwe (ZEC) usiku wa August 2 2018 imetangaza matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Zimbabwe, baada ya uchaguzi mkuu kufanikiwa kufanyika salama July 30 2018.
Emmerson Mnangagwa wa Zanu-PF ameshinda Urais wa Zimbabwe katika uchaguzi wa kwanza wa Urais, baada ya Robert Mugabe kuondoka madarakani, Mnangagwa ameshinda kwa kupata zaidi ya aslimia 50 ya kura zote dhidi ya mpinzani wake Nelson Chamisa kutoka MDC.
ZEC wametangaza kuwa Emmerson anashinda kiti hicho kwa kupata ushindi wa asilimia 50.8 ya kura zote halali zilizopigwa wakati mpinzani wake wa karibu kutoka MDC Nelson Chamisa akipata asilimia 44.3 ya kura zote.
Social Plugin