Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Vurugu Zimbabwe : MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI


Mtu mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi katika Mji Mkuu wa Zimbabwe, Harare, wakati Jeshi lilipoungana na Polisi katika kutuliza mamia ya waandamanaji wanaopinga uchaguzi mkuu wa nchi hiyo wakidai sio wa haki.

Polisi hao wamerusha maji ya kuwasha na mabomu ya kutoa machozi ili kuwatawanya waadamanaji, huku helikopta za jeshi zikizunguka angani, ambapo makabiliano hayo yameripotiwa nje ya makao makuu ya Tume ya Uchaguzi.

Wafuasi wa upinzani waanadaiwa kukosa subira kufuatia Tume hiyo kuchelewesha kutangaza matokeo ya Urais katika uchaguzi huo unaoitwa wa kihistoria uliofanyika siku ya Jumatatu baada ya miongo minne ya utawala wa Rais Robert Mugabe.

Aidha pamoja na madai hayo ya upinzani kuituhumu tume hiyo kwa upendeleo, Tume hiyo imepinga tuhuma hizo ambapo imesema inatarajia kutangaza matokeo ya Urais hapo kesho.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa, ametoa wito kwa wananchi kuwa watulivu na kuonesha ukomavu na zaidi ya yote kulinda amani na usalama wa taifa hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com