Watoto pacha walioungana tumboni na kifuani waliolazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza wamefariki dunia leo Agosti Mosi.
Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Abel Makubi amesema watoto hao wamefariki kwa tatizo la upumuaji.
Pacha hao walizaliwa Julai 25 katika Hospitali ya Sekotoure na baadaye wakapelekwa Hospitali ya Bugando, walikolazwa ICU.
Akizungumzia hali za pacha hao wiki iliyopita Dk Makubi alisema watoto hao Angelina Ramadhani (34) mkazi wa Nyakato jijini Mwanza, wameungana sehemu ya kifua na tumbo.
“Baada ya jopo la madaktari kuwafanyia uchunguzi, limebaini kwamba wanachangia moyo mmoja, mshipa mmoja unaorudisha damu kwenye moyo (inferior venacava), ini moja na kwamba viungo vilivyobaki kama mapafu, figo, tumbo kila mtoto ana vyake.”amesema Dk Makubi.
Social Plugin